Saturday, November 24, 2012

Mr Chuzi, COSOTA, TAFF kupambana na wizi wa filamu


   
   Kiongozi wa kampuni ya Tuesday Enteertaiment Limited, Mr Tuesday Kiangala 'Mr Chuzi' aesema anakuwa bega  kwa bega
na COSOTA na TAFF  kuhakikisha wanadhibiti na kupabana na haki za wasanii  zinazoibiwa kila siku.

Akizungumza ofisini kwake  baada ya kikao kilichofanywa, Peacock Hotel, ambacho kiliongwazwa na COSOTA na rais wa shirikisho la wasanii 'TAFF'
alisema  yeye akiwa kama msabazaji na tengenezaji filamu atahakikisha haki ya wasanii  zinapatikana.

Aidha alisema  kazi nyingi za wasanii  zimekuwa zikitumiwa ovyo, bila ya wasaniii  kufaidika na kile wanachokifanya, huku wakitumia ghalama kubwa
katika utengenezaji wa kazi.

"Mimi nikiwa kama msambazaji na mtengenezaji, naweza kusema naathirika mojakwa moja na wizi wa kazi za wasanii" alisea.

Katika kutano huo walikuwa pia wakijadili  ni jinsi gani wataweza kupanua soko la filamu Tanzania, ili wasanii waweze kujipatia kipato kikubwa.